Tylor na Travis penzini

Tylor na Travis penzini

Nyota wa soka la NFL Travis Kelce na mwanamuziki Taylor Swift wamekuwa katika vichwa vya habari kwa wiki nzima ikidaiwa kuwa wawili hao wako katika mahusiano ambayo yanakuwakwa kasi kwa siku za hivi karibuni.

Miezi michache iliyopita camera zilimnasa Travis akihudhuria katika tamasha la Taylor kwa lengo la kwenda kumpatia namba ya simu mrembo huyo kwa kutumia bangili ya shanga iliyoandikwa namba hiyo ingawa hakupata nafasi ya kuonana nae.

Kwa mujibu wa TMZ inaeleza kuwa licha ya mwana-soka huyo kutofanikiwa kumpa namba mwanamuziki huyo wakati alivyo maliza kutumbuiza jukwaani lakini Taylor bado alipata ujumbe na haikuchukua muda mrefu na tetesi za wawili hao kuwa na mahusiano zikaanza kuvuma.

Licha ya wawili hao kuhusishwa kuwa katika mahusiano lakini wenyewe mpaka sasa hawajithibitisha kuwa ni wapenzi, huku mashabiki wakiamini kuwa ni wazi kuna kitu kinaendelea kati ya wawili hao.

Mnamo Septemba, Taylor alijitokeza kwenye mchezo wa ‘soka’ wa Chiefs na alionekana akiwa na marafiki na familia ya Travis, na wakati ‘timu’ ya Travis ilipocheza huko New Jersey mnamo Oktoba, Taylor alihudhuria huku wakionekana wanaukaribu mkubwa na Travis.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags