Tyla ndani ya Met Gala kwa mara ya kwanza

Tyla ndani ya Met Gala kwa mara ya kwanza

Mwanamuziki kutoka nchini Afrika Kusini Tyla naye amekuwa ni miongoni wa mastaa waliyohudhuria katika usiku wa tamasha la mitindo nchini Marekani liitwalo ‘Met Gala’ ambapo na yeye alionekana akiwa ametupia vazi la mchanga lililobuniwa na Balmain kutoka Paris.

Wakati wa tamasha hilo mwanamuziki huyo alipata wasaa wa kuzungumza na media ya #Vogue ambapo aliweka wazi kuwa vazi lake ni la mchanga lijulikanalo kama ‘Sand of time’ huku akiweka wazi kuwa amefurahi sana kuwa mmoja wa wasanii waliofika katika tamasha hilo na kupiga picha.

Hii ni mara ya kwanza kwa msanii huyo kufika katika tamasha hilo kubwa, na amekuwa miongoni mwa mastaa waliyohudhuria kutokana na kujulikana zaidi kupitia ngoma anazozitoa moja wapo ikiwa ya ‘Water’ ambayo pia ilifanikiwa kuondoka na tuzo kubwa ya Grammy 2024.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags