Tyla asitisha ziara yake

Tyla asitisha ziara yake

Mwanamuziki kutoka nchini Africa Kusini Tyla ambaye alijulikana zaidi kupitia wimbo wake wa ‘Water’ ameripotiwa kughairisha ziara yake ya kwanza ulimwenguni kutokana na kupata changamoto ya kiafya.

#Tyla ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa #Instagram siku ya jana Alhamisi 7, 2024 ambapo ameweka wazi kuwa hayuko vizuri kiafya kwani hivi majuzi alikabiliwa na maumivu makali katika jeraha alilonalo na kumfanya achukue uamuzi mgumu wa kusimamisha ziara hiyo.

Hata hivyo mwanamuziki huyo hajaweka wazi kuhusiana na jeraha hilo lakini ameeleza kuwa anaendelea kupata matibabu kutoka kwa madaktari na wataalamu wa tatizo alikuwa nalo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags