Tunda Afunguka kushikiwa Bastola kwenye mahusiano

Tunda Afunguka kushikiwa Bastola kwenye mahusiano

Ebwana eeeh!! Baby mama wa  Msanii Whozu Cappucino Tunda   Amefunguka Naye Kuwahi Kupitia Katika Mapenzi Ambayo Aliwahi Mara Kadhaa Kushikiwa Bastola Na Aliyekuwa Mpenzi Wake Pale Tu Anapokuwa Amekosea Bila Kujali Ukubwa Wa Kosa,

Tunda ameandika hayo kupitia kwenye mtando wa kijamii mara baada ya tukio la Swalha kupigwa risasi na mume wake   huko jijini Mwanza na kuachia ujumbe huu mzito.

"R.I.P beautiful! .nimeskiliza hii story hadi mwili umenisisimka aisee!..aya mambo yapo kweli imenikumbusha nyuma huko na mimi nilishawahi kuwa kwenye mahusiano ambayo nikikosea kitu hata kama sio kikubwa cha kuongea tu au alikua akihisi tu kitu ni napigwa hadi nashikiwa bastola sio mara moja wala mara mbili lakini mimi ni muoga sana ilinipelekea kuacha kila kitu na mapenzi yote niliyokuwa nayo lakini nikaona hapana inabidi nitoke huku iki ni kifoooo!..

Jamani uhai ni zawadi ambayo huwezi kupewa mara mbili ikiisha imeisha haiwezi kurudiwa!..tuweni sana makini na awa tunawaita maboyfriend au wanaume zetu ukiona kama kuna vitu haviko sawa aisee ni bora uachane huko!.

Pia hata serikali hawa watu wanakabidhiwa silaha inabidi wachunguzwe sana jamani watu wanapoteza familia zao ni huzuni sana Aisee sio kikawaida kama tunavosoma tu juu huku mitandaoniMungu atupe mwisho mwema kila mmoja wetu!..mapenzi ni furaha na burudani isiwe sababu ya maumivu kwa familia zetu''






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags