Tumia kipaji ulichonacho kujiingizia kipato

Tumia kipaji ulichonacho kujiingizia kipato

Habari za wakati huu kijana mwenzangu ambaye umekuwa ukitufatilia dondoo hii ya Karia inayokujia kwa lengo la kujuzana na kuelimishana mambo mbalimbali.

Leo nimeona ni vema kushirikishana juu ya namna ambavyo kijana wenzangu utaweza kugeuza kipaji ulichojaaliwa na Mungu kuwa kazi itakayokuingizia kipato.

Najua neno hili kipaji wala sio geni kwako na kwangu mimi  nalielezea kama karama, kipawa au uwezo wa kufanya kitu chochote alionao mtu hasa vijana.

Uwezo huo unaweza kuwa ni wa asili (wa kuzaliwa nao) au wa kutafuta kama kwa kujifunza, wakati mwingine talanta huelezwa kama kipaji alichonacho mtu, kwa mfano kipaji cha uimbaji, ualimu, uandishi, uongeaji, uchungaji, udaktari na mengineyo.

Kijana wenzangu, ukweli ni kwamba kila mtu anamiliki kipaji chake  mwenyewe na kipaji hicho kinaweza kufanana na cha mwingine ila upekee unakuja kutokana na uamshwaji na ufanyiaji kazi wa kipaji husika.

Kwa mfano, leo unaweza kuwa na kipaji cha kuimba na mwenzako ana kipaji hicho hicho cha kuimba. Kwa ujumla wake tunasema mna karama ya uimbaji au talanta ya uimbaji.

Nyote mnaweza kuimba ila mmoja akaonekana ni zaidi ya mwingine...kwa nini? Ni kwa sababu tu ya upekee wa neno/kitu  ndani ya mtu kwani kila mtu anamiliki talanta yake mwenyewe tofauti kabisa na mwingine.

Kipaji cha mtu ni kama alama za vidole vya mtu (fingerprint) kwani ijapokuwa mikono na vidole vya watu wote vinaweza kuwa vinafanana bado kila mtu anakuwa na alama zake mwenyewe tofauti na za watu wote duniani.

Basi kama tumeyatambua hayo nataka kukueleza wewe kijana kwamba unapaswa sasa kutumia kipaji ulichopewa kujiingizia kipato na kujiendeleza kimaisha.

Kama wewe Mungu amekubariki kuwa mchoraji mzuri basi chora picha nyingi na tafuta fursa ya kwenda kuzuia ili upate fedha za kujikimu pindi unapokuwa chuoni.

Au kama wewe umebarikiwa kuwa daktari hakikisha unaifanya kazi hiyo kwa uaminifu na bidii kwani si kazi rahisi kuokoa maisha ya mwanadamu pindi anapougua.

Pamoja na hayo nikujuze njia za kushinda hofu na kuzidisha talanta yako kuwa juu maana wengi ushindwa kuendelea kutokana na kukabiliwa na hofu hiyo.

Kwanza unapaswa kutambua kuwa talanta yako inaweza kukupatia fedha hivyo unachopaswa kufanya ni kuifanyia kazi ili iweze kukuletea mafanikio.

Katika fani zingine, ili kupata fedha kwa talanta yako, unahitaji kuonekana, waalike wateja na uzungumze juu ya kile unaweza kufanya, hata ujisifu mwenyewe, na hii ni ngumu sana.

Kwa hivyo, kwa mfano, wanasaikolojia, wapiga picha, wasanii, ni muhimu kuzungumza juu ya talanta zao na kushiriki ubunifu na uzoefu wao na watu muda mrefu kabla watu hawajapendezwa, kujibu na kutaka kuingiliana. 

Ni muhimu kuwa wa kwanza kuzungumza, kuwaambia na kuonyesha kile kinachofurahisha kwako ili watu wenye maadili sawa watakuja, ambao kazi yako itakuwa ya thamani.

Hii inahitaji kiasi fulani cha kujitangaza na uwezo wa kujionyesha, na wengi hawana ustadi kama huo. Ni muhimu kuangalia ikiwa mtu ana marufuku ya kujisifu mwenyewe na kupenda kile anachofanya kazi yake






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags