Trump atabiri vita ya tatu ya dunia

Trump atabiri vita ya tatu ya dunia

Rais wa zamani wa Marekani Donald John Trump,  aliyetumikia kiti cha Urais kuanzia Mwaka 2017 mpaka 2021 siku ya Jana amezua Gumzo baada ya Kuandika "WORLD WAR III" kwenye Mtandao wake wa "Truth Social" aliouanzisha Mwaka 2021 baada ya Account yake ya Facebook na Twitter kufungiwa.

Mara Nyingi Donald Trump amekuwa akidai kwamba kama angekuwa madarakani vita baridi na matukio mbalimbali ya vita yanayoendelea sehemu mbalimbali za dunia yasingetokea maana anajua dawa yake.

posti hiyo imeacha maswali mengi vichwani mwa watu wakijiuliza kuwa, Je kitu gani hasa kimefanya Trump aandike maneno hayo, Je anatabiri kwamba vita ya tatu itatokea au ameandika ili aongelewe tu kama ilivyokawaida ya watu wengine.

haya haya watu wangu wa nguvu je wewe binafsi unadhani ni kweli  vita ya tatu ya dunia inaweza kutokea? Dondosha komenti yako hapo chini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags