Trela ya reality show ya The Kardashians yawashitua mashabiki

Trela ya reality show ya The Kardashians yawashitua mashabiki

Trela inayoendelea kusambaa kupitia mitandao ya kijamii ya reality show ya familia maarufu nchini Marekani ‘The Kardashians on Hulu’ imewashitua mashabiki baada ya Krish Jenner kudai kuwa ana tatizo la kiafya.

Kupitia trela hiyo Krish Jenner amewafahamisha binti zake kuwa miezi kadhaa iliyopita alikutana na daktari wake ambaye aligundua kuwa ana uvimbe mdogo ambapo haijawekwa wazi ni uvimbe wa nini.

Aidha kufuatia na taarifa hiyo iliwashitua watoto wake Khloe Kardashian, Kylie Jenner, na Kendall Jenner, huku baadhi yao wakitoka na machozi. The Kardashians on Hulu’ inatarajiwa kuanza kuoneshwa tena Mei 23 mwaka huu.

Krish Jenner ni mama wa watoto wafanyabiashara na wanamitindo maarufu Kylie Jenner, Kim Kardashian, Kendall Jenner, Khloé Kardashian, Kourtney Kardashian, Rob Kardashian aliyowapata na marehemu mumewe Robert Kardashian.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post