Tory atamani kurudi mtaani, Wanasheria wampambania

Tory atamani kurudi mtaani, Wanasheria wampambania

Baada ya ombi la kwanza la kutaka dhamana kutoka kwa ‘rapa’ Tory Lanez na kukataliwa, mwanamuziki huyo bado hajakata tamaa inaelezwa kuwa timu yake ya wanasheria imewasilisha ombi jingine la kuomba dhamana na kuachiliwa.

Ikiwa ni wiki kadhaa tangu Tory kuwekwa gerezani ripota wa Mahakama ya Meghann Cuniff ‘ame-share’ baadhi ya nyaraka zilizowasilishwa mahakamani kwa lengo la kuomba kuachiwa huru.

Wakili wa Tory Lanez, Daystar Peterson amewasilisha ombi la kuachiliwa kwa dhamana huku wakisubiri rufaa ya hukumu yake katika ‘kesi’ ya kumpiga risasi Megan Thee Stallion.

Licha ya kuwa waliwahi kuwasilisha ombi kama hilo lakini lilikataliwa na jaji wa mahakama ya Los Angeles, David Herriford mwezi September.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags