Tory ahofia kupoteza maisha akiwa gerezani

Tory ahofia kupoteza maisha akiwa gerezani

Ikiwa ni takribani wiki moja tangu msanii wa Hip-hop kutokea nchini Marekani Tory Lanez aanze kutumikia rasmi kifungo cha miaka 10 katika gereza la North Kern State  lililipo Delano mjini California.

Inadaiwa kuwa nyota huyo ameanza kuingiwa na hofu juu ya usalama na maisha yake kwani anahisi anaweza kuuawa muda wowote.

Hii ni kutokana na gereza hilo kuwa na wahalifu wakiwemo majambazi sugu na waliohukumiwa kwa makosa ya mauaji.  Inaelezwa Tory Lanez amekuwa akimwaga machozi kila mara huku akiwa hana rafiki akiohofia uhai wake.

Kwamujibu wa vyombo vya habari nchini humo vinaeleza kuwa gereza hilo lina takribani wafungwa 4,000 na kumekuwa na taarifa za mauaji ya wafungwa.

Mwaka huu mwezi Februari mfungwa aitwaye Juan Villanueva aliuawa na mfungwa mwenzie kikatili ambaye alifahamika kwa jina Ramon Escobar na mwingine aitwaye Ricardo Saldivar alikutwa amefariki kwenye chumba chake Julai 4 mwaka huu hivyo hali hiyo imekuwa ikimtia wasiwasi msanii huyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags