Tolani adai kutishiwa maisha na mashabiki wa Wizkid

Tolani adai kutishiwa maisha na mashabiki wa Wizkid

Mwingizaji na nyota wa Big Brother Naija, kutoka nchini Nigeria, Tolani Baj amedai kutishiwa maisha na mashabiki wa #Wizkid.

Tolani ameyasema hayo katika kipindi cha ‘Bahd And Boujee Podcast’  kwa kueleza kuwa alipokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa mashabiki wa Wizkid kwa sababu ya kuwa upande Don Jazzy ambaye ni msanii na mtayarishaji wa nyimbo nchini humo.

"Nilipokea vitisho vya kifo kutoka kwa mashabiki wa Wizkid baada ya kuwa upande wa Don Jazzy” amesema.

Utakumbuka April 29 Wizkid kupitia ukurasa wake wa X  alidai boss huyo wa rekodi ya Mavin hawezi kuwa producer bali ni mshawishi (Influencer) jambo ambalo lilizua taharuki katika mitandao ya kijamii.

 Tolani Baj mwenye umri wa miaka 30 amewahi kuonekana kwenye movie kama ‘Teni’s Big Day’, ‘Mercy Line’, pia amewahi kushiriki mashindano ya Big Brother Naija mwaka 2020.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags