Tiwa alipiga mswaki mara sita kabla ya kumbusu Andrew

Tiwa alipiga mswaki mara sita kabla ya kumbusu Andrew

Mwanamuziki nchini Nigeria Tiwa Savage ambaye kwa sasa ameifuata ndoto yake ya uigizaji ameweka wazi kuwa alipiga mswaki mara sita kabla ya kushuti kipande cha kukisi na mwigizaji mwenziye katika filamu yake ya kwanza ya ‘Water & Garri’.

Wakati akiwa kwenye mahojiano yake na BET, aliweka wazi kuwa siku yake ya kwanza kwenda kushuti alipewa 'sini' ya kumbusu mwigizaji mwenzie ambapo alidai kuwa alifurahi kwa sababu ilikuwa ni mara yake ya kwanza na ndipo akaingia kwenye chumba chake cha kubadilishia nguo na kupiga mswaki mara sita.

Hata hivyo, alieleza kuwa aliamua kufanya hivyo kwa sababu alitaka kuiwakilisha ipasavyo 'sini' hiyo. Savage ambaye aliigiza mhusika mkuu kwa jina la (Aisha) kwenye filamu hiyo, alishiriki busu na Andrew Bunting, mwigizaji mwenzake ambaye alipewa jina la (Kay).

Ikumbukwe kuwa filamu ya 'Water & Garri' ilioneshwa kwa mara ya kwanza kupitia Prime Video Mei 10, 2024. Filamu hiyo ilitayarishwa na Tiwa Savage wenyewe na rekodiwa huko Cape Coast, nchini Ghana, huku ikiongozwa na director Meji Alabi.

Nyota wa filamu hiyo ni Tiwa Savage (kama Aisha), Andrew Bunting (kama Kay), Mike Afolarin (kama Mide), na Jemima Osunde (kama Stephany).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags