Tisheti ya Rihanna yachanganya mashabiki

Tisheti ya Rihanna yachanganya mashabiki

Mwanamuziki na bilionea wa kwanza kutoka katika visiwa vya Barbados, Rihanna amezua hofu kwa mashabiki baada ya kuvaa 'tisheti' iliyoandikwa nimestaafu

Rihanna alivaa tishati hiyo siku ya jana wakati akiwa kwenye matembezi na mpenzi wake A$AP Rocky, vazi hilo lilikuwa limeandikwa ‘I AM RETIRED’ ikiwa na maana amestaafu.

Kutokana na vazi hilo mashabiki pamoja na wadau mbalimbali wanaokubali muziki wake wameingiwa na hofu huku wakiamini kuwa huenda Riri alistaafu muda mrefu ndiyo maana hajatoa albumu mpya hadi sasa.

Ikumbukwe kuwa siku mbili zilizopita Rihanna alizindua nywele mpya iitwayo ‘Fenty Hair’ ambayo itapatikana katika chapa yake ya urembo ya ‘Fenty Beauty’ ambapo kupitia ukurasa wake wa X (zamani twitter) aliandika

“Nywele zangu daima zimekuwa sehemu kubwa ya kazi yangu na mageuzi ya kibinafsi, na Fenty Hair iliundwa ili kuendana na nywele na mtindo wetu wa maisha, huku tukiimarisha na kurekebisha nywele zetu kila mara kwa kila matumizi”


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post