Tisa wafariki katika ajali, Katavi

Tisa wafariki katika ajali, Katavi

Watu tisa wamefariki na wengine 30 kujeruhiwa kutokana na ajali iliyotokea katika Mlima mkali wa Nkondwe, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi baada ya basi lenye namba za usajili T506 DHH kampuni ya Komba's kupinduka na kudondokea bondeni.

Taarifa ya Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Dk. Alex Mrema imesema vifo hivyo tisa vimetokea papohapo ambapo kati ya waliofariki Wanaume ni watano, Watoto watatu na Wanawake ni wanne akiwemo mjamzito.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Ali Makame amesema ajali hiyo imetokea March 6, 2023 jioni “Baada ya kufika katika Mlima huo gari liliserereka na kudondokea kwenye bonde kubwa lenye kina cha Mita zisizopungua 75”

Amesema hadi sasa chanzo cha ajali hakijajulikana na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi huku zoezi la kuitambua miili likiendela kwa ajili ya taratibu nyingine.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags