Tiktok yashtakiwa kwa kosa la kuingilia taarifa binafsi za mtumiaji

Tiktok yashtakiwa kwa kosa la kuingilia taarifa binafsi za mtumiaji

Mtandao maarufu dunia Tiktok umeshtakiwa kwa kupotosha kuhusu ulinzi wa taarifa binafsi ambaapo mwanasheria mkuu wa jimbo la  Indiana amesema mtandao huo unawapotosha watumiaji wake hasa watoto kuhusu kiwango cha maudhui yasiyofaa na usalama kwa mtumiaji

Katika malalamiko yaliyowasilishwa na Todd Rokita ambaye ni wakili mkuu wa republican amesema tiktok inakusanya maelezo nyeti na ya binafsi kutoka kwa watumiaji lakini inawahadaa kuwa taarifa zao ziko salama

Chama cha republican kimeituhumu tiktok kuwa inaingilia taarifa binafsi za mtumiaji ikiwemo historia ya kivinjari na eneo. jeshi la marekani pia limepiga marufuku tiktok kutumiwa kwenye vifaa vyake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post