Tid awajia juu wasanii wa singeli

Tid awajia juu wasanii wa singeli

Na Habiba Mohammed 
Aloooooo! Ama kweli ule msemo unaosema ukisema cha nini wenzio wanajiuliza watakipata sio maneno yangu basi bwana mashabiki wa mziki wa singeli na baadhi ya waimbaji kumjia juu yule mwamba wa kitambo kidogo Tid kudharau mziki huo.

Msanii huyo katika mahojiano yake na moja ya chombo cha Habari alikataa kutumia mic akidai kuwa mic ya mtangazaji huyo inatumiwa sana na wasanii wa mziki wa singeli hivyo sio hadhi yake. 

Kitendo hicho ambacho kiliibua mjadala katika mitandao ya kijamii kikitafsiriwa kama  dharau kwa wanamzikii wa singeli na baadhi ya wasanii wa muziki huo hawakukaa kimya waliamua kumjia juu na kumjibu kutokana na kitendo alichokifanya. 

Aidha haikuishia hapo mwanangu sana yule kijana ni mbishi akaamua kurudisha mashambulizi kwa wasanii hao kupitia video yake ambayo ilikuwa na ujumbe unaosema kuwa “nilikuwa najaribu kuweka point tu ila sitaki mtu anitishie nimefanya ninachoweza kufanya na nimesema nilichotakiwa kusema msinitishie, am too humble’ amesema Tid 

Mwanangu sana embu ndondosha komenti yako hapo chini je ni sawa msanii kudharau kazi za wasanii wengine? Na je lengo la Tid halikuwa la kuwadhalilisha kama alivyo sema, usiache kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kwa Habari za motrooo na uhakika kama hizi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags