The Rock Aitupilia mbali  fast & farious 10

The Rock Aitupilia mbali fast & farious 10

Ebwana eeh!! unaambiwa MuigizajiDwayne Johnson maarufu  “The Rock”  amekataa ombi la kurejea kuigiza muendelezo wa filamu ya Fast & Furious sehemu ya 10.

Mwezi Novemba mwaka huu muigizaji Mark Sinclair “Vin Diesel” kupitia ukurasa wake wa instagram alimuomba The Rock arudi kumalizia sehemu ya mwisho ya Fast & Farious kwa ajili ya mashabiki wao na kutimiza ahadi yao kwa marehemu Paul Walker.

The Rock katika interview yake na CNN iliyochapishwa siku ya jana amekataa ombi la Vin Diesel kurejea katika Fast & Farious na kumkosoa kwa kitendo chake cha kuongolea suala hilo katika mitandao ya kijamii kwa kuwahusisha watoto na marehemu Paul Walker.

Nilishangazwa sana na post ile ya Vin Diesel, mwezi wa sita mwaka huu niliongea nae faragha na kumwambia sitaweza kuigiza tena filamu hiyo ila nitatoa ushirikiano wangu katika kuandaa filamu hiyo ili kuhakikisha inafanikiwa na hata washirki wengine wote niliongea nao na walinielewa.” Majibu ya The Rock

The Rock ameweka wazi msimamo wake hatarudi tena katika Fast & Furious na anawatakia kila kheri.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags