TFF watoa onyo kwa wanaoshirikiana na waliofungiwa

TFF watoa onyo kwa wanaoshirikiana na waliofungiwa

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limewakumbusha kwa mara nyengine wadau wa mpira wa miguu kuwa ni kosa kushirikiana na watu ambao wamefungiwa kwa makosa mbalimbali yanayo husiana na kukiuka kanuni na taratibu za mpira.

Limesema kuwa ni muhimu kuzingatia utaratibu wa adhabu kwa wadau husika waliofungiwa badala ya kwenda kinyume na katiba, kanuni na taratibu zinazosimamia mpira wa miguu.

Aidha shirikisho hilo linaendelea kufuatilia ukiukaji huo ili kuchukua hatua stahiki sambamba na waliofungiwa wanajiweka katika hatari ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu iwapo hawatatumikia adhabu zao kikamilifu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags