Tetemeko la ardhi Indonesia vifo vyafika 160

Tetemeko la ardhi Indonesia vifo vyafika 160

Maafisa wa huduma za dharura nchini Indonesia wanaendelea kuitafuta miili zaidi ya watu kutoka kwenye vifusi vya nyumba na majengo yaliyoangushwa na tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu wapatao 162 katika kisiwa cha Java.

Tetemeko hilo la ardhi lilifikia kipimo cha 5.6. na lilirindima hadi mji mkuu wa Indonesia, Jakarta. Gavana wa Java magharibi Ridwan Kamili alitoa taarifa ya vifo vya watu hao kwa masikitiko makubwa. Pia amesema watu wengine wapatao 326 wamejeruhiwa katika maafa hayo.

Ameeleza kuwa miongoni mwa watu waliokumbwa na maafa ya tetemeko walikuwa wanafunzi. Kwa mujibu wa taarifa tetemeko hilo la ardhi limetokea kwenye sehemu ambapo watu wengi wanaishi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags