Tesa wa Huba afariki dunia

Tesa wa Huba afariki dunia

Mwigizaji Grace Mapunda maarufu kama ‘Tesa’ amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Novemba 2, 2024 akipatiwa matibabu katika chumba cha wagonjwa mahututi, kwenye Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania, Chiki Mchoma amesema mwigizaji huyo awali aliugua kwa muda mrefu kisha akarudi kwenye hali ya kawaida na kuendelea na majukumu yake kama kawaida, ndipo juzi alikimbizwa hospitalini hadi umauti ulimkuta.

"Alikuwa anaumwa akakimbizwa Hospitali ya Mwananyamala, kwa bahati mbaya umauti ukamkuta hapo alikuwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi. Hadi kufikia usiku wa kuamkia leo umauti ukamkuta, "amesema Mchoma.

Mwigizaji mwenzake, Jacob Stephane 'JB' amesema atamkumbuka Grace kwa ucheshi na utendaji kazi wake.

"Katika waigizaji wa kike, Grace alikuwa ni kati ya waigizaji wazuri na wakubwa sana, mcheshi, mara ya mwisho nilimuona jana hospitali, hatukuweza kuzungumza alikuwa ICU,’’ amesema JB.

Endelea kufuatilia Mwananchi Scoop kwa taarifa zaidi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags