Terry Joyce afariki dunia

Terry Joyce afariki dunia

Aliyekuwa mwigizaji wa vichekesho kutoka nchini Marekani Terry Joyce ambaye amewahi kuonekana katika kipindi cha Byker Grove na BBC Hebburn amefariki dunia.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Sun News imeeleza kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 81 alijenga upendo kwa watu na kujiongezea heshima kutokana na umahiri wake akiwa katika kazi yake ya sanaa.

Terry alianza kuigiza mwanzoni mwa miaka ya 90 katika kipindi maarufu cha BBC kama Gerry akuiwa pamoja na wa igizaji wenziye kama Chris Ramsey, Gina McKee, Vic Reeves na Jason Cook. 

Pia alikuwa katika kipindi cha televisheni ‘Super Gran na Spender’ ambayo ilikuwa ni programu ya #JimmyNail, ambayo iliendeshwa kwa safu tatu kutoka 1991 hadi 1993.

Hivi karibuni kabla ya kifo chake aliigiza katika ‘BBC Sitcom Hebburn’, ambayo alichukua uhusika wa wakili.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags