Teknolojia ya kuwakutanisha marehemu na ndugu zao

Teknolojia ya kuwakutanisha marehemu na ndugu zao

Shirika la Utangazaji la Munhwa (MBC) nchini Korea limezindua teknolojia mpya itakayo saidia familia kukutana tena na watu wao wa karibu waliyofariki dunia.

Ili kutilia maanani suala hilo shirika hilo limetoa filamu fupi iitwayo ‘I Met You’ ambayo ilimkutanisha mama aitwaye Jang Ji-sung, na binti yake aliyefariki kwa saratani ya damu mwaka 2016.

Klipu ya dakika tisa ya filamu hiyo ikimuonesha Jang akiongea na mwanaye imepata maoni zaidi ya milioni 13 kwenye mtandao wa YouTube huku baadhi ya wadau wakikosoa filamu hiyo kama unyonyaji wa maumivu ya kibinafsi.

Aidha kutokana na baadhi ya watu kuwa na mtazamo chanya watayarishaji walitetea filamu hiyo wakisema kuwa nia yao ilikuwa ni kuzifariji familia ambazo zimepoteza ndugu zao pamoja na kukuza teknolojia ya uhalisia.

Hata hivyo baada mwanamama huyo kuzungumza na binti yake alitoa maoni kwa kueleza kwamba programu hiyo inaweza kuleta faraja kwa wengine ambao wamepoteza wapendwa wao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post