TCRA yaonya vyombo vya habari kurusha maudhui kuhusu dini

TCRA yaonya vyombo vya habari kurusha maudhui kuhusu dini

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imeonya vikali vyombo vya utangazaji nchini humo zikiwemo Radio na Televisheni kuacha kurusha maudhui ya kufikirika hasa yanayogusa imani za dini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA onyo hilo limetokana na kuzagaa kwa video fupi kuhusu masuala mbalimbali ya imani ya dini.

Ingawa taarifa haikuwekwa wazi moja kwa moja ni maudhui gani hasa  lakini katika siku za hivi karibuni zimezagaa video (clip) kwenye mitandao zikimuonyesha mchungaji Dianna Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi kutoka mkoani Mwanza, akisema alienda mbinguni na kueleza mambo kadhaa aliyokutana nayo mbinguni.

Aidha kauli hizo ambazo zimeleta mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii, likiongelewa na wengi kama jambo lisilowezekana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags