TBT: Unakumbuka movie ya Kuch Kuch Hota Hai

TBT: Unakumbuka movie ya Kuch Kuch Hota Hai

Hehehe! Make hapa kwanza ncheke   wadau wa mwananchiscoo leo bwana nimewaamisha kidogo  kuoka kwenye muziki kuja katika movie , enzi hizo bwana Tv iko kwa mtu mmoja tuu kitaani basi utaskia asie oga asiingie humu wazee wenzangu nazani mnanielewa

Leo bwana katika Throuback Tuesday (TBT) tunakurudisha nyuma kidogo nimekusogezea kile kigongo cha movie ambacho kilijulikana katika mataifa mbalimbali na kupendwa na watu wa kila rika ambayo ni “Kuch Kuch Hota Hai” (something happens) kutoka katika soko la Bollywood. Ambapo watu wengi huifahamu kama KKHH au K2H2.

Movie hii imetoka rasmi October 16  mnamo mwaka 1998  kwa nafasi kubwa imejaa vichekesho na mapenzi ambayo iliandikwa na kuongozwa na Karan Johar na kutayarishwa chini ya Dharma Productions. 

Aidha move hiyo imeigizwa na watu mashuhuri katika secta ya uigizaji nchini India ambao ni Shah Rukh Khan na Kajol katika filamu yao ya nne pamoja na Rani Mukerji, na Salman Khan. Mpaka sasa wakali hao bado wanashika nafasi za juu kupitia tasnia hiyo ya uigizaji.

 Eeeeeeeeeeeh! sasa wanangu wa @mwanachiscoop shusha comment hapo chini utuambie ni movie gani unayo ikubari kutoka kwa wakali hao na huichoki kuitazama kila siku






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags