TBT: Unaikumbuka sumu ya penzi ya Belle 9

TBT: Unaikumbuka sumu ya penzi ya Belle 9

‘Sumu ya penzi ukishailamba hata kwa maziwa huwezi kupona, siyo kama mimi nakukataa ila moyo wangu unasita, wazazi wangu watanishang’aa nyumbani wewe ulishatoroka.’

Hii ni sehemu ya mashairi yenye hisia za kutosha kutoka kwenye Ngoma ya Sumu ya Penzi ya msanii Abednego Damian maarufu kama Belle 9.

Ni zaidi ya miaka 11 iliyopita tangu ngoma hii itoke, lakini bado melodi na midundo yake inasikika. Ni miongoni mwa ngoma za zamani (TBT) za Bongo Fleva zinazosikilizwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii.

Hiyo ni kutoka kwa mwanamuziki mkali wa RnB Bongo Belle 9 kufanya vema na kupangilia mashairi katika ngoma hiyo.

Kwa kuweka kumbukumbu sawa, Belle 9 aliweza kutoka kimuziki mwaka 2009 akitokea Mji Kasoro Bahari, Morogoro pale Mtaa wa Mafinga.

Belle 9 alitoka na Sumu ya Mapenzi kisha Masogange ambazo zilimtambulisha vizuri kwenye medani ya Bongo Fleva.

Baada ya Sumu ya Penzi na Masogange, Belle 9 alikiwasha kinoma na ngoma nyingine kama Wewe ni Wangu, Nilipe Nisepe, Umenitupa, Ladha ya Mapenzi, House Boy, Wanitaka, Burger Movie Selfie, Umefanana Naye, Vitamin Music, Wewe Nami, Listen, Shauri Zao, Amerudi na nyingine kibao (ni zaidi ya 50).

Leo ndani ya jarida letu amekuwa TBT wa wiki kupitia ngoma yake hiyo ya Sumu ya Penzi. Tunakupenda Belle 9 na tunatamani kusikia ngoma yako nyingine mpya kwa mwaka huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags