TBT:  Unaikumbuka ‘starehe’ ya msanii Ferooz

TBT: Unaikumbuka ‘starehe’ ya msanii Ferooz

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Feruzi Mrisho maarufu kama Ferooz aliyepata kutamba na kundi la Daz Nundaz lililokuwa na maskani yake Sinza Dar es Salaam leo katika TBT anatukumbusha mbali hasa wimbo wake ule wa Starehe aliyomshirikisha msanii Professor Jay.

Msanii huyu ni kazi ya wale ambao walikuwa wakiingiza fedha nyingi kupitia muziki mpaka pale alifanikiwa kununua gari lake aina ya Jeep.

Ferooz ni moja kati ya wasanii walioitikisa vichwa vya habari katika tasinii hii ya muziki wa bongo fleva miaka ya nyuma kwa sauti yake kali ya kulalamika.

Kati ya vibao au nyimbo zilizomuweka kwenye ramani na kumpatia umaarufu mkubwa msanii ferooz ni wimbo wa starehe aliomshirikisha msanii mwenzake Professor Jay.

Unaambiwa katika wimbo huo, kazi ya kuundaa beat ilifanyika bongo records kwa P Funk Majani.

Nyimbo hii iliteka hisia za watu wengi kutoka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kwa ujumbe ulioimbwa ndani ya wimbo huo.

Ujumbe ulikuwa unahusu gonjwa hatari la ukimwi lilivyohatari na kumfanya Raisi mstaafu wa awamu ya tatu kwa sasa ni marehemu, Hayati Benjamini Mkapa kufurahishwa na kuahidi kumpatia zawadi.

Taarifa ambazo ziliwahi kusambaa mtaani ni kwamba Rais Mkapa alimpatia zawadi ya gari aina jeep kwa kuthamini mchango wake na kuheshimu kile anachokifanya, lakini msanii huyo alipofanyiwa mahojiano alikataa kwamba hakuwahi kupewa gari bali hilo wanaloliona watu alijinunulia mwenyewe nchini Dubai.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags