TBT: UNAIKUMBUKA MABINTI WA KITANGA

TBT: UNAIKUMBUKA MABINTI WA KITANGA

Mwanamuziki wa bongo fleva, Joseph Rushahu ‘Bwana Misosi’ aliyewahi kutamba na kibao cha ‘Mabinti wa Kitanga’ leo ameweza kuwa TBT wetu.

Huyu mtu alikuwa hasikiki kwa muda sana kutokana na majukumu mengine, lakini mwaka 2020 aliibuka na wimbo wake mpya wa Makofi kwa hayati Magufuli.

Bwana Misosi aliitikisa vilivyo nchi kwa nyimbo zake za Nitoke Vipi aliomshirikisha Hard Mad na huu wa Mabinti wa Kitanga aliomshirikisha Mwana FA, lakini kamanda huyu alikuwa kimya kwa muda mrefu kabla ya hivi karibuni kutoka na ngoma ya Makofi kwa Magufuli.

Bwana Misosi alishawahi kusikika akisema kuwa amejipanga kurudi upya ndiyo maana ameamua kuachia project ya Makofi kwa Magufuli, na mwakani ataachia ngoma kibao tu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags