Taylor Swift auza ndege yake

Taylor Swift auza ndege yake

Baada ya kuzuka sintofahamu kupitia mitandao ya kijamii kuhusiana na ndege binafsi ya mwanamuziki Taylor Swift kudukuliwa na mwanafunzi wa Florida, na sasa inadaiwa kuwa Taylor ameuza ndege hiyo aina ya ‘Dassault Falcon 900’.

Inaelezwa kuwa ndege hiyo aliyokuwa akiitumia toka mwaka 2009 imeuzwa katika shirika la Missouri huku ikimuacha Taylor na ndege moja aina ya Dassault 7X yenye uwezo wa kubeba abiria wengi zaidi.

Uuzwaji huu unakuja baada ya ndege aliyobaki nayo kukabiliwa na changamoto katika upitishwaji wa hewa ambapo inasemekana kuwa ameuza ndege hiyo kwa lengo la kununua carbon ili kuirekebisha Dassault 7X.

Hivyo basi Swift atendelea kumiliki ndege moja aina ya ‘Dassault Falcon 7X’, inayokadiriwa kuwa na thamani ya $54 milioni ambayo ni zaidi ya tsh 136 bilioni.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post