Taylor Swift aomboleza kifo cha shabiki

Taylor Swift aomboleza kifo cha shabiki

Mwanamuziki Taylor Swift anaomboleza kifo cha shabiki kilichotokea dakika chache kabla ya kupanda stejini katika tour yake ya Eras Tour iliyofanyika Brazil usiku wa kuamkia leo.

Kupitia Instastory yake ametoa taarifa hiyo ya kumpoteza shabiki na kutoa pole kwa familia ya shabiki huyo ambaye ni binti wa miaka 23 aliyefahamika kwa jina la Ana Clara Benevides.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa shabiki huyo alifariki alipofikishwa hospitali baada ya kupata mshituko wa moyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags