Tausi: Naumia mwanangu akitaniwa kuhusu mwonekano wangu

Tausi: Naumia mwanangu akitaniwa kuhusu mwonekano wangu

Muigizaji wa Filamu Nchini Tausi Mdegela  Amefunguka juu ya changamoto za unyanyasaji anazokumbana nazo mitandaoni, kazini pamoja na mitaani kutokana na muonekano wake ambao ni mfupi kwa kimo.

Mwigizaji huyo ameyasema hayo kupitia mahojiano na moja ya chombo cha habari kuwa kitu kinachomuumiza zaidi ni jinsi Mwanae wa Kike anavyotaniwa kisa Muonekano wake.

“kumlea mtoto peke yako ni changamoto kuna wakati mwingine anasema mama mbona wanasema wewe ni kadogo inamaanisha kuwa hakupenda jambo hilo lakini ndo hivyo atazoea hatuwezi kubadilisha’” amesema Tausi.

Mbali na hayo ameeleza juu ya hatima yake ya uigizaji na kusema kuwa ana Mwaka wa Pili hajaitwa na Muandaaji wa Filamu yeyote kwa ajili ya kuigiza hivyo anajishikiza na Biashara ili aendeleze maisha na Mtoto wake.

Chanzo BBC


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post