Tanzania yaingiza wasanii nane tuzo za Afrimma 2021

Tanzania Yaingiza Wasanii Nane Tuzo Za Afrimma 2021

Na Aisha Lungato

Jumla ya wasanii nane kutoka Tanzania wamefanikiwa kuingia katika tuzo za “The International Award and Home of the Africa Voice maarufu kama Afrimma.

Idadi hiyo ya wasanii ikiongozwa na msanii maarufu Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ambaye jina lake limetajwa kwenye vipengele sita katika tuzo hizo kubwa barani Afrika.

Wasanii wengine walioingia katika tuzo ni Rajabu Abdul maarufu Harmonize, Rayvanny, Alikiba, Zuchu, Rosa Ree, Nandy pamoja na Darasa.

Wengine kwa upande vipngele mbalimbali kama vile DJ, Watayarishaji bora wa muziki na waandaaji bora wa video, Tanzania imefanikiwa kupata wawakilishi ambao ni Dj Sinyorita, Director Kenny pamoja na Lizer aka lizrclassic.

Jana waandaaji wa tuzo hizo wametoa orodha rasmi ya wasanii watakao wania tuzo katika vipengele mbalimbali.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post