Tanzania yachaguliwa kufanya filamu na South Korea

Tanzania yachaguliwa kufanya filamu na South Korea

Tanzania imechaguliwa kuwa nchi ya kwanza Africa kufanya filamu na South Korea kwa ajili ya kuunganisha soko la filamu la Tanzania na Korea.

Hayo yameelezwa kupitia ukurasa wa Instagram wa Mwigizaji mkongwe Steve Nyerere ambapo amedai kuwa kauli hiyo ilitolewa na Rais wa filamu Korea Kusini Yang Jongkon walipokuwa wakifanya naye mazungumzo.

“Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuunganisha soko la filamu la Tanzania na Korea basi nami sina budi kusema wazi kuwa Tanzania ndio nchi ya kwanza tutakayoshirikiana nayo tutakapoingia Africka. Kwa sasa tunamalizia kuimarisha Bara la Asia kwenye tasnia hii ya filamu,” alinukuu Stive kauli ya Rais huyo

Aidha katika taarifa hiyo iliyotolewa na Stive imeeleza kuwa Rais YANG Jongkon ameahidi kufika Tanzania kuonana na wasanii wa Tanzania akiongozana na baadhi ya watengeneza filamu wa Korea pamoja na kuhakikisha anaendelea kuudumisha na kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Korea Kusini.

Utakumbuka kuwa wasanii wa filamu Tanzania wapo Korea kwa takribani siku ya tatu sasa katika ziara yao ya kujifunza mambo ya filamu.

Baadhi ya mastaa waliyopo kwenye ziara hiyo ni Irene Paul, Wema Sepetu, Idris Sultani, Dorah, Johari Chagula, Steve Nyerere, Eliud Samwel, Getrude Mwita, Gabo Zigamba na Godliver Gordian.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Steve imeeleza kuwa wasanii hao wamefanikiwa kutembelea studio kubwa za Busan kwa ajili ya kuona jinsi filamu za Kikorea zinavyotengenezwa, filamu hizi maarufu zinazotambulika kama Kdrama (Korean Drama).


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post