Takribani 14 wafariki kwa kuangukiwa na bango la tangazo

Takribani 14 wafariki kwa kuangukiwa na bango la tangazo

Imeripotiwa kuwa takibani watu 14 wamefariki dunia siku ya jana Jumatatu Mei 13, 2024 baada ya kuangukiwa na bango la matangazo kufuatiwa na mvua iliyonyesha jijini Mumbai nchini India.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini India vimeeleza kuwa mpaka kufikia siku ya leo Jumanne Mei 14, 2024 Kikosi cha Kitaifa cha Kukabiliana na Maafa kiliopoa miili 14 na kuwaokoa manusura 74.

Aidha Afisa wa NDRF Nikhil Mudholkar aliambia vyombo vya habari vya ndani kwamba manusura 31 tayari wameruhusiwa kurudi katika majumba yao huku wengine wakiendelea na matibabu hata hivyo katika maelezo yake ameweka wazi kuwa bado kuna watu wanahofiwa kukwama lakini juhudi za uokoaji bado zinaendelea.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags