Taarifa kutoka TFF kuhusu sakata la Kisinda

Taarifa kutoka TFF kuhusu sakata la Kisinda

Alooooooh! Mambo yameshakuwa yamotroo, baada ya malalamiko mengi shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF imetoa maelezo kuhusiana na ishu ya winga wa yanga Tuisila Kisinda kupigwa stop, shirikisho hilo limeweka wazi na kusema kuwa.


Usajili wa wachezaji wa kigeni, hasa kwa klabu ambazo timu zao zinacheza mashindano ya kimataifa ulishapitishwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji katika mazingira maalumu ilishughulikia haraka usajili wa wachezaji hao wa kigeni ili wawahi usajili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Wachezaji wote wa klabu hizo za Azam, Geita Gold, Simba, na Yanga walishapewa leseni zao kwa ajili ya msimu wa 2022/2023 ambazo pia ndizo zimetumika kuwaombea usajili kwa ajili ya mashindano ya CAF.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 62(1) ya Ligi Kuu Toleo la 2022, klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12. Hivyo, klabu kutaka au kujaribu kusajili wachezaji zaidi ya idadi hiyo ni kwenda kinyume na kanuni.

Oooohoooooooh! Dondosha komenti yako hapo chini mtu wangu wa nguvu una lipi la kuzungumza kuhusiana na sakata hili.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags