T.I na mkewe wafutiwa mashitaka

T.I na mkewe wafutiwa mashitaka

Mkali wa ngoma ya ‘Live Your Life’, T.I na mkewe Tinny Harris wameripotiwa kufutiwa mashitaka yaliyokuwa yakiwakabili ya unyanyasaji wa kingono waliyoyafanya mwaka 2005 dhidi ya mwanamke ambaye jina lake halijawekwa wazi.

Utakumbuka kuwa Januari mwaka huu mwanamke mmoja kutoka Marekani alifungua kesi mahakamani wanandoa hao kwa kudai kuwa walimlewesha pombe na kisha ‘Rapa’ huyo kumuingilia kinguvu huku mkewe akiwa anamkandamiza kitandani.

Aidha kwa mujibu wa hati iliyotolewa mahakamani inaeleza kuwa licha ya kutupilia mbali shauli hilo lakini kesi hiyo inaweza kufunguliwa tena baadaye na mtuhumiwa endapo atapata ushahidi wa kutosha.

Hii sio mara ya kwanza kwa ‘rapa’ huyo kuhusishwa katika kesi mbalimbali, utakumbuka kuwa katika miaka ya hivi karibuni zaidi ya wanawake 30 wameripotiwa kumshutumu T.I kwa kuwanyanyasa kingono lakini mpaka leo hajawahi kufikishwa katika vyombo vya sheria kutokana na kutokuwa na ushahidi wa kufanya atiwe nguvuni.

Hata hivyo wiki hii T.I aliponea kwenye tundu la sindano ambapo alishikiriwa na polisi katika uwanja wa Ndege wa Atlanta ‘Hartsfield-Jackson’ baada ya utambulisho wake kudaiwa kuwa sio sahihi, lakini masaa machache baadaye aliachiwa huru.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags