Suge hataki kusikia habari za kutoa ushahidi kuhusu kifo cha Tupac

Suge hataki kusikia habari za kutoa ushahidi kuhusu kifo cha Tupac

Mtayarishaji mkongwe na CEO wa zamani wa Death Row Records, Suge Knight amedai kuwa hatopanda kizimbani kutoa ushahidi wa aliyemuua Tupac Shakur pamoja na kudaiwa kuwa alikuwa pembeni ya Tupac kwenye gari siku ambayo anashambuliwa kwa risasi Jijini Las Vegas, Septemba 7 mwaka 1996.

Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ ambayo walifanya naye mahojiano, Suge Knight amefunguka kuwa hatatoa ushahidi dhidi ya Keffe D ambaye amekamatwa week iliyopita akihusishwa na mauaji hayo.

Licha ya rafiki huyo wa marehemu Tupac kukataa kusimama kizimbani kwa kutoa ushahidi, amedai kuwa muuaji wa Tupac Shakur siyo ambaye polisi wanamdhania.

Kauli hizo za Suge zimeibua maswali mengi kwenye vichwa vya wafuatialiji wa kesi hiyo, wengi wakihoji kwamba inawezekanaje akashindwa kutoa ushahidi kwenye mauaji ya aliyekuwa mtu wake wa karibu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags