Suge aendelea kumkalia kooni Diddy, Ray J amtetea

Suge aendelea kumkalia kooni Diddy, Ray J amtetea

Mwanzilishi mwenza wa rekodi lebo ya ‘Death Row Records’ kutoka Marekani Suge Knight, ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 28 jela atoa angalizo kwa Diddy juu ya kutumia jina la Brother Love.

Akizungumza katika podcast yake ya Collect Call With Suge Knight, inayoruka moja kwa moja kutoka gerezani amesema jina hilo ambalo Diddy amekuwa akilitumia kwa muda mrefu halitoweza kumsaidia chochote pindi awapo gerezani.

“Usitumie jina Brother Love ukiwa gerezani, hilo siyo jina zuri la utambulisho huko ndani,”
Hata hivyo, Suge alieleza kuwa maisha ya Diddy yako hatarini kwa sababu anafahamu siri nyingi kuhusu biashara hiyo ya ngono.

“Puffy, maisha yako yako hatarini kwa sababu unajua siri za nani anayehusika na kile chumba kidogo cha siri mnachoshiriki mambo yenu. Unajua watajaribu kukumaliza kama wataweza. Nilijisalimisha mwenyewe. Wakati mwingine lazima ukubaliane na hali halisi, mara nyingi ndiyo njia bora,” alisema.

Utakumbuka kuwa hii siyo mara ya kwanza kwa Suge kumzungumzia Diddy mwezi Juni kupitia Podcast yake hiyo alidai Diddy anafanya kazi na FBI kwa muda mrefu.Ndiyo maana linapokuja suala lake la kisheria mambo yanakuwa tofauti huku akidai kuwa wapo baadhi ya watu wanalifahamu hilo wakiwemo rafiki zake wa karibu pamoja na timu yake nzima.

Mbali na hayo ya Suge mwanamuziki Ray J ameonekana kumkingia kifua Diddy kwa kueleza kuwa hakuna chochote kinachohusiana na uhalifu kilichokuwa kikifanyika katika sherehe za msanii huyo kama inavyodaiwa licha ya kuwa amehudhuria sherehe zake nyingi.

“Hatukuwahi kuona mambo yanayosemwa sasa, na sijawahi kuwa kwenye chumba ambacho watu wanadai kilikuwa na hayo mambo, na sikuwahi kufahamu kuwa kilikuwepo."

Diddy alikamatwa Jumatatu Septemba 16, na kuzuiwa katika gereza linaloitwa ‘The Metropolitan Detention Center (MDC) kwa tuhuma za ulaghai wa kingono na usafirishaji wa binadamu ili kujihusisha na biashara hiyo ya ngono.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags