Suge adai Akon alimbaka binti wa miaka 13

Suge adai Akon alimbaka binti wa miaka 13

Mtayarishaji mkongwe wa muziki kutoka nchini #Marekani, #SugeKnight amedai kuwa mwanamuziki na mfanyabiashara #Akon, kwamba aliwahi kumbaka binti wa miaka 13.

Akiwa katika mahojiano na #DavidMayers kupitia #Podcast yake mpya ya ‘Collect Call’ #SugeKnight amesema ugomvi wake na Akon haukuwa kwa sababu ya pesa, bali tukio la kumbaka binti wa miaka 13 ambaye ni mtoto wa rafiki yake.

Aidha #Suge alidai kuwa si huyo tu bali hadi mtayarishaji wa muziki #Detail alihusika katika tukio hilo ambapo aliweka wazi kuwa kulikuwa na binti mwingine mwenye miaka 12 ambaye #Detail alimfanyia ukatili huo wa kijinsia.

Baada ya kugundulika hilo, dada wa binti huyo alitaka kwenda polisi lakini kutokana na ukaribu ambao #Suge alikuwa nao kwa #Akon, ilibidi amshauri wayamalize kiutu uzima.

Ikumbukwe kuwa wawili hao kabla ya kuwa na bifu walikuwa na rafiki wa karibu.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags