Stoute: Gomez alimtumia Rema, kurudisha umaarufu wake

Stoute: Gomez alimtumia Rema, kurudisha umaarufu wake

Mfanyabiashara na CEO wa ‘UnitedMasters’ Steve Stoute kutoka nchini Marekani amedai kuwa mwanamuziki Selena Gomez alimtumia mkali wa Afrobeat Rema kurudisha umaarufu wake.

Wakati akiwa kwenye mahojiano na Podcast ya ‘Afrobeats Intelligence’ aliweka wazi kuwa mwanamuziki huyo kutoka Marekani aliutumia wimbo wa ‘Calm Down’ ambao alishirikishwa na Rema kurudi katika game ya muziki, huku akidai kuwa haikuwa na ulazima kutoa remix ya wimbo huo kutokana na wenyewe kuwa mkubwa.

Remix ya ‘Calm Down’ iliachiwa rasmi mwaka mmoja uliopita, ambapo mpaka kufikia sasa inazaidi ya watazamaji milioni 794 kupitia mtandao wa #Youtube, ambao pia ulifanikiwa kuchukua tuzo ya MTV katika kipengele cha ‘Best Afrobeat song’.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post