Steve Nyerere;Jamanii tuishi na watu vizuri.

Steve Nyerere;Jamanii tuishi na watu vizuri.

Na Habiba Mohammed

Ebwanaa mambo vipi? Basi bhana kwenye mitandao ya kijamii kumetaradadi sio powa, staa wa bongo movie Steve Nyerere ameandika ujumbe kuntu kama tunavyojuaga yeye muda wote hudondosha madini tuu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ukisomeka kuwa "Kuomba ni Aibu, kuomba ni fedheha ,na kunyimwa ni kudhalilika tujifunze kusaidiana bila kupigiana magoti na tuishi na watu vizuri ila usiwaamini sana” ameandika Steve Nyerere

Alooooh! Pia bwana akaongezea kwa kusema kuwa “Maana leo watakusisitiza Maisha ni Safari lakini kesho hao hao watakunyima nauli” amesema mzee wa ya nini mie Steve

Hayaa haya wanangu wa faida ,wewe unaishi vipi na watu wanaokuzunguka? Je unahisi kuna sababu yoyote imemfanya staa huyo kuandika ujumbe huo kwenye ukurasa wake? Dondosha comment yako hapo chini, au sio shida zako.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post