Steve Nyerere: hukumu ni kazi ya mungu

Steve Nyerere: hukumu ni kazi ya mungu

Mchekeshaji maarufu hapa nchini, Steve Nyerere ametoa ujumbe mzito ambao umewataka watu kukumbuka kwamba hukumu ni kazi ya Mwenyezi Mungu pekee.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Steve Nyerere ameandika “Tumekuwa watu wa kuhukumu na tukisahau kazi hiyo ni ya Mwenyezi Mungu….tunajibebesha mamlaka makubwa sana na tunasahau mamlaka madogo ya maisha yako na familia yako yanakushinda.

“Yapo mambo tumetendewa na binadamu wenzetu mpaka unajiuliza huyu ni binadamu kweli, upaswi kuweka tunasamehe maana yote mabaya uliotenda na imani Munyu aliyehai aliyaona nay eye anasema nitakujibua kwa wakati ninaopennda mimi,” ameandika Steve Nyerere na kuongeza

“Kwenye maisha yetu mambo mengi tunajifunza kutoka kwa binadamu wenzetu hawa hawa akuna hapa duniani aliyezaliwa na roho mbaya  hakuna, hakuna aliyeumbwa na roho mbaya wala na fedha, wala aliyezaliwa na kuambiwa utakuwa tajiri au utakuwa Mh,”

Hayo ni baadhi ya maneno aliyoandika Steve leo katika ukurasa wake wa Instagram.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags