Steve Nyerere amkosha Msigwa Tamasha la Faraja ya Tasnia

Steve Nyerere amkosha Msigwa Tamasha la Faraja ya Tasnia

Ikiwa zimebaki siku tano kufikia kilele cha tamasha la "Faraja Ya Tasnia" linalohusisha kuwakumbuka wasanii waliofariki dunia lililoandaliwa na mwigizajia Steve Nyerere, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa ametoa pongezi kwa mwigizaji huyo kwa kuwakumbuka waliotangulia mbele za haki.

Msigwa ameyasema hayo akitoa ‘comment’ kwenye video ya maandalizi ya tamasha hilo iliyochapishwa na msanii Steve katika ukurasa wake wa Instagram leo Jumatatu Septemba 2, 2024.

"Jambo muhimu, twendeni tukawape faraja. Kudos Tivu ake, akili mingi we Mhehe," ame-comment Msigwa 

Tamasha hilo litakuwa la kwanza nchini kuwakumbuka wasanii waliotangulia mbele ya haki.

Akizungumza na Mwananchi Steve alisema litakuwa likifanyika mara moja kwa mwaka na kwa 2024 litafanyika Septemba 7 katika Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam bila kiingilio.

Huku likiambatana na ibada ya kuwaomba marehemu kutoka kwa mchungaji Mwamposa pamoja na Shekhe wa Mkoa, kupiga nyimbo zao, kutoa zawadi za pole ndugu wa marehemu pamoja na chakula cha pamoja






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags