Stars yaahidiwa bilioni 1.3 wakiipiga Congo

Stars yaahidiwa bilioni 1.3 wakiipiga Congo

Wachezaji wa ‘timu’ ya Taifa ya #TaifaStars na ‘benchi’ la ufundi wameahidiwa tsh 1.3 bilioni endapo itafuzu hatua 16 bora ya fainali za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika #AFCON.

Stars leo wanatarajia kurudi tena uwanjani katika mchezo dhidi ya  ‘timu’ ya Taifa #DRCongo saa 5.00 usiku kwenye Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly nchini Ivory Coast katika mchezo wa mwisho wa kundi F wakiwa na alama moja baada ya  Jumapili kutoka sare ya bao 1-1 na Zambia.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mwanaspoti, leo, Januari 24, 2024, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro amesema ahadi hiyo ya fedha imetolewa ili kuongeza hamasa kwa wachezaji.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags