Spyro awaumbua wanaosema diamond kaiga wimbo wake

Spyro awaumbua wanaosema diamond kaiga wimbo wake

Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu wadau wa muziki kumshambulia Diamond kwa ku-copy nyimbo za wasanii wengine ikiwemo wimbo wa mkali kutoka Nigeria Spyro, sasa mkali huyo kamkingia kifua #Mondi na kuwaumbua wanaotoa maneno.

Kupitia mtandao wa Tweeter #Spyro ame-tweet akipinga kuhusiana na wanaodai #Diamond ka-copy wimbo wake, akiwata waache kumshambulia #Simba, na kueleza kuwa kila mtu anatoa mawazo kutoka sehemu nyingine.

Huku akidai kuwa watu wakubali au wakatae ukweli ni kwamba hakuna mwenye chake wote wanatoa mawazo kutoka sehemu nyingine, Diamond ni mshikaji wake kwa hiyo watu wamuache, ukizingatia yeye na #Simba wametoa ngoma ya pamoja na inafanya vizuri.

Ikumbukwe kuwa #Diamond ameshirikishwa kwenye wimbo wa #Spyro uitwao For You ambao humo ndani wapo wasanii wengine kutoka #Nigeria akiwemo Teni na Iyanya






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags