Sophia: Davido hana malezi mazuri

Sophia: Davido hana malezi mazuri

Mpenzi wa zamani wa mwanamuziki Davido na mzazi mwenzie Sophia Momodu amedai kuwa hakubaliani na msanii huyo kupewa malezi ya mtoto wao aitwaye ‘Imade’ kwani Davido hana malezi mazuri.

Wakati akiwasilisha hoja hizo Mahakamani Sophia aliwasilisha ushahidi wa kifo cha mtoto wa Davido na Chioma ‘Ifeanyi’ aliyefariki mwaka 2022 kwa kuzama kwenye Bwawa la kuogelea nyumbani kwao na kueleza kuwa malezi ya staa huyo ni hatari kwa mtoto wao.

Hata hivyo mwanadada huyo aliongezea kwa kudai kuwa ameongeza kwa sasa Davido ameoa mwanamke mwingine hivyo malezi ya mtoto wao hayatokuwa salama huku akiiomba mahakama isitoe idhini ya Davido kumlea mtoto huyo.

Mbali na hayo Sophia aliendelea kwa kusisitiza kuwa kutokana na kazi ya Sanaa ya msanii huyo amekuwa mtu wa kusafiri na nyumbani kwake kumekuwa na marafiki wengi wakiume hivyo kitendo hicho siyo salama kwa mtoto wao wa kike.

Kwa upande wa Davido alinyoosha mikono juu na kukubali yaishe baada ya marehemu mwanaye kuingizwa katika kesi hiyo huku akikubali kumwachia malezi ya mtoto wao.

“Unaleta mada ya kifo cha mtoto wangu kila likija swala la madai ya malezi ya mwanangu huku ukijua swala hilo linatuumiza mimi na mke wangu kila siku kwenye maisha yetu.

Imade atakuwa mkubwa na ataona jinsi nilivyompambania kwa sasa wewe kuwa nae kwani mwanangu hawezi kuwa mtoto kila siku atakuwa tu” ameandika Davido


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post