Sonko ahaidi kufanya vurugu katika uchaguzi

Sonko ahaidi kufanya vurugu katika uchaguzi

Kiongozi wa upinzani nchini Senegal, Ousmane Sonko, hana mpango wa kutafuta maridhiano, na Rais Macky Sall, na ameashiria kuwa anaweza kujaribu kuvuruga uchaguzi wa mwaka ujao, ikiwa hataruhusiwa kugombea.

Sonko aliyasema hayo nyumbani kwake katika mji mkuu wa Dakar, ambako amekuwa chini ya kizuizi cha nyumbani, tangu alipohukumiwa kifungo cha miaka miwili, mwezi Juni, kwa mashtaka yaliyotokana na madai ya ubakaji.

Kiongozi huyo amekanusha mashtaka hayo na kusema kuwa yanalenga kumzuia kushiriki katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi Februari, 2024.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags