Sonia Monalisa akataa kusoma bongo

Sonia Monalisa akataa kusoma bongo

Ohooo kimeumana huko mitandaoni unaambiwa mtoto wa msanii maarufu hapa nchini,Yvone Cherrie maarufu Monalisa, Sonia ameweka wazi kuwa atasomea nje ya nchi elimu yake ngazi ya chuo.

Mtoto huyo anayetambulika kwa jina la Sonia Monalisa amesisitiza kuwa  hakuna chuo chochote  anachokifahamu hapa nchini. 

Maelezo hayo ameyatoa katika mahojiano yake na chombo kimoja cha habari na kueleza kuwa tayari mama yake alimtengenezea mazingira ya kisaikolojia kuwa hatokuja kusomea Chuo kikuu hapa bongo.

‘’Mama yangu ameshani tengenezea mazingira ya  kisaikolojia kuwa sitokuja kusomea  chuo hapa bongo, kwahiyo toka niko kidato cha nne  nilijua kabisa sitasoma bongo yaani hata vyuo vya bongo sivijui “amesema na kuongeza

 “Huwezi amini yani najua tu kama  kuna (UDSM) lakini vingine sijui kwasababu mama yangu alishaniambia nikuache usomee hapa nikasema hapana kwasababu anawajua walimwengu bora niepukane na shari za walimwengu anipeleke huko  nikatulize akili’’ amesema.

Hata hivyo maneno hayo yameibua mzozo katika mitandao ya kijamii ambapo watu wengi wanesema kauli hiyo aliyoitoa ya kutojua vyuo vya bongo si ya kweli.

Najua na wewe mtu wangu una maoni yako, tuambiee na wewe unaungana na Sonia hufahamu chuo chochote bongo? Tuambie comment yako hapo chini!

 






Comments 5


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags