Son aomba radhi kukataa kushika Iphone, Akilinda mkataba wake

Son aomba radhi kukataa kushika Iphone, Akilinda mkataba wake

Mchezaji wa ‘klabu’ ya Tottenham Hotspurs, Heung Min-Son ameomba radhi kwa shabiki aliyemuomba kupiga naye picha na kisha kukataa kuishika simu ya shabiki huyo aina iPhone kwa sababu anamkataba wa ubalozi na kampuni ya Samsung, ambao unambana kufanya hivyo.

Nahodha huyo ambaye ni raia kutokea Korea Kusini ameingia mkataba wa ubalozi na Samsung na haruhusiwi kushika kifaa chochote ambacho ni bidhaa shindani na kampuni ya Samsung kutokana na mkataba wake.

Licha ya hayo mchezaji huyo anaruhusiwa na kampuni hiyo kupiga picha (Selfie) na Shabiki akiwa na simu ya kampuni nyingine nje ya Samsung pasipo yeye kuishika simu hiyo kama alivyoombwa na shabiki huyo.

Hata hivyo ilimbidi Son apige picha (selfie) na shabiki huyo kwa kutumia simu nyingine ya Samsung na kukubali kuishika.
.
.
.
#MwananchiScoo
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags