Snura: Sio muziki tuu hata kwenye filamu hamtaniona

Snura: Sio muziki tuu hata kwenye filamu hamtaniona

Moja ya stori ambazo zilishika vishwa vya habari vingi siku ya jana ni kuhusaiana na suala zima la mwanamuziki Snura Anton Mushi 'Snura' akitangaza kuachana na muziki, lakini leo akizungumza na Mwananchi amesema sio muziki tu bali hata filamu hatashiriki, yaani kwa ujumla yeye na sanaa ndio basi tena.

Amesema kazi hizo zichukuliwe kama hazijawahi kuwepo. Ameondoka huko na harudi tena.

"Mimi nimeacha sanaa zote nilizowahi kuzifanya zikiwemo hizo za muziki na filamu."

Hata hivyo, kuhusu wasanii waliowahi kuacha muziki baada ya muda wakarudi, Snura amesema hata likija dili gani hawezi kurudi.

"Mimi kama nilivyosema sababu yangu ya kuacha muziki sio kwamba sikuwa napata dili, zilikuwa nyingi sana lakini nimetangaza kuacha. Sasa sijui dili lipi ya muziki itakayoweza kuja kunishawishi. Ukweli, nimeacha sababu ya Allah, sasa sijui hizo dili za muziki kama zitakuwa na umuhimu sana kuliko Allah. Siwezi kurudi huko nawahakikishia watu ambao hawaniamini."

Snura amesema ukimya wake wa muda mrefu ni kwa sababu hakutaka kujihusisha tena na muziki na hakutaka kutangaza kabla ya sasa kuamua kufanya hivyo ili watu wajue na nini anajihusisha nacho sasa.

"Nina miaka miwili sijafanya kazi ya muziki, nilishaiacha na mwanzoni nilikuwa na wazo la kuacha kimya kimya, ndiyo maana imefika hiyo miaka miwili. Watu mlikuwa mnaniona kimya, lakini kuna vitu vilisababisha kuona kuna sababu ya kuzungumza ndiyo maana nimezungumza sasa. Kitu kinachoniingizia riziki kwa sasa, najishughulisha na kilimo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags