Simba yatemana na Okrah

Simba yatemana na Okrah

Klabu ya Simba imethibitisha kuachana na aliyekuwa mchezaji wao raia wa Ghana, Augustine Okrah baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa msimu mmoja.

Okrah alijiunga na Simba mwezi Julai mwaka 2022 akitokea klabu ya Bechem United ya nchini Ghana kwa mkataba wa miaka miwili.

Pia amewahi kuzitumikia klabu za Asante kotoko ya Ghana, Al Hilal ya Sudan pamoja na North East United ya nchini India.

Pamoja na hayo kumekuwa na sintofahamu na kutokuwekwa bayana sababu za kusitishiwa mkataba wake mpaka sasa huku tetesi zikidai kuwa ni utovu wa nidhamu ndio uliopelekea kiungo huyo wa Ghana kupoteza nafasi kwenye klabu hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags