Siku ya Muziki ya Kimataifa, unapenda kusikiliza ngoma za aina gani

Siku ya Muziki ya Kimataifa, unapenda kusikiliza ngoma za aina gani

Kwa wapenzi wa burudani katika upande wa muziki, leo ni siku yao maalumu kwani dunia inaadhimisha siku ya Muziki ya Kimataifa.

Uwepo wa siku hiyo uliidhinishwa na aliyekuwa Rais wa Baraza la Muziki la Kimataifa (UNESCO), Lord Yehudi Menuhin kwa kuandika barua kwa wanachama wa IMC akitangaza tarehe 1 Oktoba kuwa itakuwa Siku ya Muziki ya Kimataifa.

Barua hiyo iliambatana na sababu za kuadhimishwa kwa siku hiyo ni pamoja na Kuimarisha kukuza sanaa ya muziki katika sekta zote za jamii, Kuhamasisha utekelezaji wa itikadi za UNESCO za amani na urafiki miongoni mwa watu, Kuhamasisha kuthaminiwa kwa tamaduni kwa pande zote, hasa thamani kwa wasanii na nyinginezo.

Jinsi ya Kusherehekea Siku ya Muziki ya Kimataifa

Kufanya tamasha na wanamuziki katika eneo lako
Katika kila eneo, kuna wanamuziki wachanga ambao wangependa kucheza mbele ya hadhira, hivyo basi unaweza kusheherekea siku hii kwa kupanga onesho katika sehemu yenye uwazi kwa lengo la kuifurahisha jamii.

Kutengeneza ukimya katika eneo unalo ishi
Pia njia nyingine unayoweza kusheherekea siku hii ni kujaribu kuwashawishi majirani zako kuzima kelele zote kwa muda ili muweze kupata muda wa kusikiliza sauti asili mfano ndege wakiruka, upepo na majani yakitoa sauti yake.

Hatua nyingine unayoweza kuifanya ili kuadhimisha siku hiyo ni kupata mwalimu wa muziki au muuzaji wa vyombo vya muziki ambaye anayeweza kutoa elimu kuhusu tasnia hiyo.

Siku ya Muziki ya Kimataifa ilianza kuadhimishwa 1 Oktoba, 1975 huku zaidi ya nchi 150 kote ulimwenguni ziliadhimisha nguvu ya muziki kuunganisha jamii na watu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags